SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgiji, rekodi zinaonyesha kuwa anaukubali ‘muziki’ wa kiungo wa Zambia, Clatous Chama, hivyo kwa timu inayowinda saini yake lazima ijipange.
Mbelgiji huyo alisema kuwa mchezaji mwenye juhudi mazoezini ndiye ambaye anampa namba jambo ambalo limekuwa likimnyima usingizi Ibrahim Ajibu ambaye kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona alijenga urafiki na benchi.
Rekodi zinaonyesha kuwa Chama ametumia dakika 1,745 huku Simba ikiwa imecheza mechi 28, Chama amecheza mechi 23, Sven akiwa amesimamia mechi 18, Chama ametumia dakika 1,213 huku kwa Patrick Aussems aliyeongoza mechi 10 alitumia dakika 532.
Mechi 11 Chama alicheza dakika zote 90 ambazo ni sawa na dakika 990 huku mechi nne akitumia dakika 223, akiwa amekosekana kwenye mechi tatu pekee chini ya Sven.Mechi za Chama mbele ya Sven hizi hapa: Lipuli (90), Yanga (90), Mbao (90), Alliance (81), Namungo (34), Coastal Union (90), Polisi Tanzania (90), JKT Tanzania (27), Mtibwa Sugar (90), Kagera Sugar (90), Biashara United (90), Lipuli (90), KMC (81) Azam (90), Yanga (90).
0 COMMENTS:
Post a Comment