April 4, 2020

KOCHA wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa kama kweli klabu hiyo inataka kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani, Heritier Makambo, anayekipiga Horoya ya Guinea kwa sasa, wafanye hivyo haraka ila wawe na uhakika wa kumlipa mshahara mzuri.

Zahera ambaye inaaminika kuwa ndiye Meneja wa mchezaji huyo, amesema kwake yeye haoni tatizo la Makambo kurudi Yanga baada ya klabu hiyo kuonyesha nia ya kufanya hivyo kwa kuwa nyota huyo alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga na itakuwa vizuri kama akirejea sehemu ambayo aliishi kama nyumbani.

Uongozi wa Klabu ya Yanga, ulithibitisha kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Luc Eymael, ameagiza kusajiliwa kwa wachezaji wanne wa kigeni, ambao ni mshambuliaji mmoja, winga, kiungo wa kati na beki mmoja, ambapo tayari GSM wameshaanza kufanyia kazi ishu hiyo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Zahera alisema: “Kama kweli Yanga wanataka kumrudisha Makambo, mimi sioni shida yoyote, kwa sababu ni mchezaji ambaye aliishi na kupendwa na mashabiki wa timu hiyo na Dar es Salaam aliishi kama nyumbani, sawa kama wanamtaka, lakini lazima wamlipe mshahara mzuri kama anaolipwa Horoya,” alisema Zahera.

Makambo aliichezea Yanga kwa msimu mmoja, 2018/19 na kufanikiwa kuifungia mabao 17 katika ligi kuu, kisha akatimkia Horoya ambako bado ana mkataba wa miaka miwili.

5 COMMENTS:

  1. Hawana jeuri yakuvunja mkataba,na endapo makambo atarudi yanga ina maana ndio hatima yake kisoka itakapo ishia kwasababu yanga ina uwezekano mdogo sana kushiriki mashindano makubwa Afrika hivyo kufanya akose exposure kwa timu kubwa ambapo ingemuwia rahisi sana kupata dili kutokana na kuonekana,all in all she is a good player aje tu ila ajipange kisaikolojia maana GSM mguu nje mguu ndani muda na wakati wowote ule anaweza akajikataa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmmh we jamaa ebu chek hivyo vingereza ccc hivyo. Pia pilipili usiyoila yakuwashian?

      Delete
  2. Zahera haache kabisa Mambo ya yanga.Tulimpa nafasi akatupiga pesa awaache wenzake muda wake umepita

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ha ha ha ha ha dude hivyo vingereza vya kebehi brother au unadhani cjui nilichoandika?kwa taarifa yako nimeandika makusudikale.

      Delete
  3. Mleteni makambo ili yanga ikae vizuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic