PAPY Tshishimbi, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa anaendelea kufanya mazoezi ili kulinda kipaji chake pamoja na kuchukau tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wapo nyumbani wakiendelea kufanya mazoezi binafsi.
Tshishimbi ambaye ni nahodha amesema:"Naendelea kujiimarisha kipindi hiki cha Corona lengo langu ni kuona kwamba tukirejea kwenye maisha ya kawaida niwe kwenye kiwango changu ama zaidi katika kuitumika Yanga," .
Yanga ikiwa imecheza mechi 27, Tshishimbi amecheza mechi 23 na ametoa pasi moja ya bao kwenye mechi dhidi ya Biashara United.
0 COMMENTS:
Post a Comment