April 21, 2020

JERSON Tegete nyota wa zamani wa Yanga anayekipiga ndani ya Klabu ya Alliance amesema kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya Corona ili awe salama.

Alliance yenye maskani yake mkoani Mwanza ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo imecheza mechi 29 kibindoni imekusanya pointi 29.

Tegete amesema:"Ikiwa hauna shughuli ya lazima ya kufanya ikiwa ni kusafiri ni busara kubaki nyumbani na kuchukua tahadhari ili uwe salama.

"Janga hili ni kubwa na ni letu sote hivyo itapendeza kila mmoja akiwa anapambana kwa juhudi kushinda hili kwani mambo sio shwari, nami nachukua pia tahadhari," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Ila hicho kajifulana alichovaa? watanzania tuwache ujinga.Wewe mwafrica Mtanzania ni juzi tu Raisi wa wamarekani kawakataa watanzania halafu unamuona mtu au Mtanzania tena maarufu amejivisha bendera ya Marekani? Kama si kujizalilisha kitu gani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic