KIUNGO wa Manchester
United, Paul Pogba, amefichua kwamba, wakati anakua, alikuwa shabiki mkubwa wa Arsenal
na hiyo ilichangiwa na kumfuatilia zaidi Mfaransa mwenzake, Thierry Henry.
![]() |
| Pogba akishangilia na Jesse Lingard ndani ya United |
Mwaka 2009, Pogba
alijiunga na United akitokea Le Havre ya nyumbani kwao Ufaransa wakati akiwa na
miaka 16, kisha akaondoka na kuelekea Juventus mwaka 2012, akarejea tena Old
Trafford kwa uhamisho ulioweka rekodi ya dunia mwaka 2016.
![]() |
| Thierry Henry (kushoto) akishangilia bao na Mfaransa mwenzake, Robert Pires walipokuwa Arsenal |
Pogba raia
wa Ufaransa, alisema, Henry alikuwa mchezaji wake kipenzi pamoja na Ronaldinho,
Ronaldo na Zinedine Zidane na wakati anaanza soka alitamani kuyafikia mafanikio
yao.
"Niwe
mkweli kabisa, nilianza kuishabikia Arsenal, hiyo yote ni kutokana na uwepo wa
wachezaji wengi kutoka Ufaransa.
"Mimi
na ndugu yangu mmoja ndiyo tulikuwa tunaipenda Arsena, lakini mwingine akawa
shabiki wa Manchester United.
"Siwezi
kusema kingine chochote zaidi ya nilikuwa nampenda Henry na kwa sababu yake
nikawa shabiki wa Arsenal.
“Baadaye
nikabadilika na kumfuata yule ndugu yangu mwingine ambaye si shabiki wa Arsenal,
nikawa naye katika kuishabikia United!"
![]() |
| Pogba akiwa na jezi za Juventus |
Pogba, 27,
msimu huu umekuwa si mzuri kwake ndani ya kikosi cha United kwani amekuwa akisumbuliwa
na majeraha ya mara kwa mara.
Msimu huu
katika Premier amecheza mechi saba tu, hajafunga bao lolote, lakini ana asisti
mbili.











0 COMMENTS:
Post a Comment