UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utatumia mfumo mpya wa kufanya usajili wa wachezaji wao ili kupata wachezaji watakaoleta ushindani ndani ya kikosi chao msimu ujao.
Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wengi wapo nyumbani wakifanya mazoezi binafsi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa watafanya mambo kipekee ndani ya msimu huu katika kuboresha kikosi chao.
"Tupo vizuri kwa sasa na tunaamini kwamba wakati ukifika tutaleta upekee wa katika mfumo wa usajili wa wachezaji wetu na mfumo utakuwa ni wa kipekee kuepuka zile janjajanja ambazo zimezoeleka.
"Kikubwa kwa sasa mashabiki watulie wasiwe na presha kila kitu kipo sawa na mambo yatakuwa vizuri wenyewe watapenda ila wasisahau pia kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona," amesema.

Hapana wasiwasi ni vizuri kubadilisha hata karibu kikosi kizima watazoweana mapema ili wachukuwe ubingwa
ReplyDelete