HASSAN Kabunda, winga wa KMC Juni 7, 2020 alimaliza msumari wake wa mwisho kwa kumtungua mlinda mlango wa Yanga bao la kideo kwa mpira wa adhabu uliomshinda Metacha Mnata wakati Yanga ikikubali kulala kwa mabao 3-0.
Mchezo wa kirafiki ulichezwa ulichezwa Uwanja wa Uhuru ambapo ushindani ulikuwa mkubwa kwa timu zote mbili.
Mchezaji wa zamani wa Yanga na mchambuzi wa masuala ya michezo, Ally Mayai amesema kuwa sababu kubwa iliyowafanya Yanga wapoteze mchezo huo ni kukosa mechi za ushindani kwa muda mrefu.
"Ilikuwa ni mechi nzuri na ngumu ila kikubwa kilichowafanya Yanga wakapoteza ni kukosa mechi nyingi za ushindani na kukaa muda mrefu bila kucheza mechi hicho ndio kimewaponza.
"Ni wachezaji wachache ambao huwa wanaweza kuendelea kwenye ubora wao iwapo watakaa muda refu bila kucheza ila KMC wao waliweza kumudu kwenye falsafa yao ambapo walianza tangu mwanzo wa mchezo, kumiliki mpira na kucheza," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment