PROSPER Pius nyota wa Transit Camp leo ameyeyusha ndoto za Klabu ya Gwambina FC kujikatia tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Bara kwa kuwatungua bao la mapema lililowafanya wagawane pointi mojamoja.
Dakika 90 kwenye mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Uhuru zilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.'
Gwambina iliyo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi B ilikuwa inahitaji pointi tatu pekee ili ijihakikishie nafasi ya kushiriki ligi.
Kwa sasa inapaswa isubiri mpaka mechi yake inayofuata na kushinda ili kufikisha jumla ya pointi 44 ambazo hazitaweza kufikiwa na mshindani wake mkubwa Geita Gold mwenye pointi 33 wote wakiwa wamecheza mechi 19.
Mkononi imebakiwa na mechi tatu ambazo ni pamoja na ile dhidi ya Pamba FC, Rhino Rangers na Mashujaa.







0 COMMENTS:
Post a Comment