YUSUPH Mlipili beki wa Simba leo ameonyesha makeke yake ndani ya Uwanja kwa muda wa dakika 18 akisherehesha ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Mwadui FC uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Mlipili aliingia dakika ya 72 akichukua nafasi ya Shomari Kapombe ambaye alikuwa kwenye ubora wake ndani ya uwanja katika dakika 72 alizocheza.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Mlipili kuanza chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ndani ya Ligi Kuu Bara.
Simba imelipa kisasi cha kutunguliwa bao 1-0 na Mwadui FC kwenye mchezo wao wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kambarage.
Mabao ya Simba leo yaliwekwa kimiani na Hassan Dilunga dakika ya tisa, Agustino Simon wa Mwadui alijifunga dakika ya 21 katika harakati za kuokoa hatari na msumari wa mwisho ulikomelewa na nahodha John Bocco.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 75 kibindoni baada ya kucheza mechi 30.







0 COMMENTS:
Post a Comment