June 10, 2020


KOCHA wa zamani wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa amekosa nafasi ya kwenda kuinoa Klabu ya Township Rollers  kutoka Goborone nchini Botswana kwa sababu hajui kuongea kiingereza.

Zahera amesema siyo timu hiyo pekee ambayo ilikuwa inahitaji huduma yake bali hata baadhi ya timu kutoka Afrika Kusini zilimpigia simu lakini yeye akagoma kwa sababu hawezi kuzungumza kiingereza na hapendi kuwa na mkalimali katika kazi zake.

Zahera amesema amepigiwa simu na mawakala kutoka Botswana akimueleza kwamba klabu hiyo inatafuta kocha na yeye wamemuona atawafaa kwa kuwa hana timu ila yeye aliwajibu kuwa hawezi kuzungumza kiingereza vizuri hivyo itakuwa ngumu kwake kuwasiliana na wachezaji pamoja na viongozi.

"Wakala kutoka Botswana alinipigia simu akaniambia kuwa Township Rollers wanahitaji kocha na wameona mimi nawafaa, lakini nikawaambia kuwa mimi siwezi kuongea kiingereza na sitakuwa huru kufanya kazi nikiwa na mkalimani na siyo hao tu, kuna timu nyingine kutoka Afrika Kusini zilikuwa zinanitaka pia," amesema Zahera.

Zahera alipigwa chini ndani ya Klabu ya Yanga mwanzoni mwa msimu huu kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu kwenye mechi za kimataifa. Nafasi yake imechukuliwa na Luc Eymael raia wa Ubelgiji.

Chanzo:Championi

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic