ARISTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa ratiba kwake imekuwa ngumu kwa kuwa ana mechi ngumu na za ushindani ikiwa ni pamoja na ile ya Simba, Julai Mosi.
Juni 14, Ciaoba atakiongoza kikosi chake kumenyana na Mbao mchezo wa ligi, atakuwa na kazi ya kumenyana pia na Simba Julai Mosi, Uwanja wa Taifa robo fainali ya Kombe la Shirikisho.
Cioaba amemesema:- "Ratiba siyo rafiki kwetu, tutakutana na Simba, mchezo ambao ni muhimu kwetu ila utakuwa mgumu kutokana na namna ambavyo kikosi changu kilivyo, imani yangu vijana wataipambania timu ili iweze kupata mafanikio."
Azam FC ni mabingwa watetezi wa kombe la Shirikisho, iwapo watapenya hatua hiyo watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Kagera Sugar ama Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment