LEO Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael itamenyana na Ndanda FC Uwanja wa Taifa mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Ndanda FC inanolewa na Kocha Mkuu, Meja Msataafu Abdul Mingange ambaye anaipambania timu isishuke Daraja ikiwa nafasi ya 15 Kwenye msimamo inakutana na Yanga iliyo nafasi ya tatu.
Mchezo wa Kwanza uliopigwa Nangwanda Sijaona, Yanga ilishinda bao 1-0 lililojazwa kimiani na Patrick Sibomana.
Hawa hapa nane wataukosa mchezo wa leo :-
Bernard Morrison anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi aliyopewa na Kamati ya Maadili mwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons.
Papy Tshishimbi bado hajawa fiti.
Mapinduzi Balama ataukosa mchezo kwa kuwa alipata majeruhi mazoezini.
Lamine Moro anatumikia adhabu ya kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Mwinyi Kazimoto Kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania.
Ally Ally, Eric Kambamba,Andrew Vincent, Ramadhan Kabwili hawapo Kwenye mpango wa mwalimu
0 COMMENTS:
Post a Comment