June 26, 2020


MABINGWA watetezi wa Simba wameanza kuivutia kasi Klabu ya Tanzania Prisons kwa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa Juni,28 Uwanja wa Sokoine.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 yaliyojazwa kimiana na John Bocco kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City.

Wapinzani wao Tanzania Prisons wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Tanzania kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

Tanzania Prisons ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Adolf Rishard hesabu zake kubwa ni kumaliza ligi ikiwa ndani ya 10 bora msimu huu wa 2019/20.

Simba inahitaji pointi tatu ili kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo wanahitaji kuutwaa ubingwa wakiwa na mechi nyingine mkononi.

Timu zote zimecheza mechi 31 ambapo zimebakiwa na mechi saba mkononi kwa sasa.

 Mchezo wao uliopita Uwanja wa Uhuru, Simba ilitoshana nguvu ya bila kufungana na Tanzania Prisons hivyo kazi itakuwa kubwa pale watakapokutana ndani ya uwanja.

Rishard amesema:"Tunahitaji kufanya vizuri mchezo wetu ujao, tutakutana na timu nzuri na ngumu ila tupo tayari."

Sven amesema:"Ni mchezo muhimu na mgumu kwetu hilo tunalitambua hivyo wachezaji wana kazi ya kusaka pointi tatu kutimiza malengo."

2 COMMENTS:

  1. Marefa wanakera na vyombo vyetu vya habari vya michezo ni hovyo kabisa kwani ishu na kelele zinakuwa mi pale tu mwamuzi anapoonekana kuteleza kimaamuzi na kuinufaisha simba ila simba ikionewa sio ishu hata kidogo. Goli la tatu la simba zidi ya mbeya city lina mapungufu gani hadi refa alikatae? Wachezaji wa mbeya city wawili kwa mpigo walikwenda kumfanyia rafu chama kwa umahiri wa chama kama professional player akawakwepa na wachezaji hao kwenda kugongana wao wenyewe.Goli likafungwa nadhani wachezaji hao wa mbeya city kwakujua walitenda foul wakaamya kufeki kuumizwa,lakini na nani? Na mchezaji mwenzake sasa simba inaadhibiwa vipi hapo? Na kwanini refa hakupuliza filimbi ya foul on the spot of action? Au alikwenda kutizama marejeo ya tv kwenye VARA?

    ReplyDelete
  2. Kwa hili la waamuzi kufanya makosa ya mara kwa mara, haswa sheria ya tafsiri ya kuotea/0ffside Ni vema wapigwe msasa ili kuongeza weledi wa namna ya kubaini/ kutafsiri makosa ya offside.. vi ginevyo itakuwa Ni mwendelezo wa aibu kwa mpira wetu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic