YUSUPH
Mhilu, mshambuliaji namba moja wa Klabu ya Kagera Sugar akiwa na mabao 12,
chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime amesema kuwa kilichowamaliza wapinzani wao Azam FC ni kushindwa kutumia
nafasi ambazo walizipata.
Kwenye
mchezo huo uliochezwa Juni 24, Uwanja wa Kaitaba, Azam FC inayonolewa na Kocha
Mkuu, Aristica Cioaba ilikubali kufungwa bao 1-0 baada ya kipa wa Azam FC,
Benedict Haule kutema mpira uliokutana na guu la Mhilu.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa ulikuwa mchezo mgumu na kila timu
ilikuwa inahitaji ushindi hivyo kosa la Azam FC lilikuwa kushindwa kutumia
nafasi walizotengeneza.
“Mchezo
ulikuwa kwenye usawa, wao walikuwa wanatushambulia nasi tulikuwa tunawashambulia,
kilichotufanya tukaweza kuwapunguzia kasi ni kosa lao moja walilofanya sisi
tukatumia na kupata pointi tatu hakuna kingine,” amesema Mhilu.
Kagera Sugar, ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 44 huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili na
pointi zake 58 zote zimecheza mechi 31.
Mhilu umeongea vizuri kwa kuwaheshimu wapinzani wenu hiyo ni safi sana kuheshimiana.
ReplyDelete