June 26, 2020




JUSTIN Shonga, mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini inaelezwa kuwa yupo mbioni kujiunga na Klabu ya CS Maritimo ya nchini Ureno, hiyo ni baada ya kushindwana na Simba.

Shonga raia wa Zambia, inaonekana ameshindwana na klabu hiyo kwa kuwa dau lake la usajili lipo juu sana. Inatajwa thamani yake sokoni ni euro 600,000 (zaidi ya Sh bilioni moja), sasa huenda hiyo ilikuwa kikwazo kikubwa kwa Simba ambayo ilikuwa imeshakubali kumlipa mshahara wa Sh mil 34 kwa mwezi, kwa mujibu wa watu wake wa karibu.

Taarifa za uhakika kutoka kwa mtu wa karibu wa mshambuliaji huyo anayeishi Afrika Kusini, zinasema kuwa mshambuliaji huyo anajipanga kuelekea barani Ulaya baada ya kupata timu hiyo kutokana na kugomea ofa za klabu za Afrika alizokuwa akipokea.

Chanzo hicho kilisema kuwa Mzambia huyo anatarajia kutimkia kwenye nchi hiyo baada ya mazungumzo yake na klabu ya CS Maritimo ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Ureno kuwa katika hali nzuri.

“Shonga amefanya maamuzi ya kubadilisha upepo kwa sababu ameamua kwenda kucheza Ulaya na atakwenda nchini Ureno kujiunga na Klabu ya CS Maritimo kwa sababu timu nyingi za Afrika zimeshindwa kufikia muafaka naye.

“Sasa hivi kumekuwa na mazungumzo na Orlando kwa kuwa bado wao ndio wanammiliki kwa sababu ya mkataba wake lakini kwa upande wa mchezaji ameonyesha utayari kwa kwenda kucheza Ureno na siyo kuendelea kucheza Afrika,” kilisema chanzo.

4 COMMENTS:

  1. Tokea mwanzo Simba hata siku moja haijafikiria mchezaji huyo

    ReplyDelete
  2. Kwa hivyo GSM si wamchukue?

    ReplyDelete
  3. Bilion moja alafu uje hapa uzingue, aende zake tuu

    ReplyDelete
  4. Chanzo hicho... Taarifa nyingine bhana, Au ni wewe mwenywe umeandika.?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic