June 27, 2020


KIKOSI cha Simba kimeedelea na mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kujiweka sawa kwa mchezo wa kesho utakaopigwa Uwanja wa Sokoine, dhidi ya Tanzania Prisons.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck inakutana na Tanzania Prisons inayonolewa na Kocha Mkuu, Adolf Rishard.

Mchezo wao uliopita walitoshana nguvu ya bila kufungana ndani ya dakika 90 wakati huo Simba ilikuwa chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems.

Mechi iliyopita ya Prisons Uwanja wa Sokoine ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Tanzania huku Simba ikisepa na pointi tatu mbele ya Mbeya City.

Ikiwa nafasi ya kwanza Simba na pointi 78 inakutana na Prisons ambao wapo nafasi ya 10 na pointi 42.

Moja ya mchezo mkali unaotarajiwa kupigwa kesho kwa kuwa Rishard ni bingwa wa kulazimisha sare huku Simba wakiwa wabovu kwenye kulazimisha sare ambapo kwenye jumla ya mechi 31 walizocheza ina sare tatu ikiwa ni timu yenye sare chache.

Prisons kwenye mechi 31 ilizocheza imelazimisha sare 15  na moja kati ya hizo 15 ililazimisha mbele ya Simba pia.

Richard amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya ushindani na lengo letu ni kupata ushindi katika mchezo wetu.

Sven amesema:"Wachezaji wapo tayari ni suala la kusubiri na kwa kuwa tunahitaji ushindi.

3 COMMENTS:

  1. Jamani kweli hii blogu inaposemwa ni haki.Makanjanja.Eti "Simba ni wabovu wa kulazimisha sare.Wametoa sare tatu tu"Kweli mwandishi anayejua kazi yake wataandika utumbo huo.Kutoa sare ni umahiri?Unapoteza pointi 2 ukitoa sare.!!!!

    ReplyDelete
  2. SOMA HIKI KIPANDE VIZURI MBONA KINAELEWEKA USIMLAUMU MTU KABLA HUJAJUA KAMAANISHA NINI MAANA KUMBE WEWE NDO HUJAPAMBANUA VIZURI''Moja ya mchezo mkali unaotarajiwa kupigwa kesho kwa kuwa Rishard ni bingwa wa kulazimisha sare huku Simba wakiwa wabovu kwenye kulazimisha sare ambapo kwenye jumla ya mechi 31 walizocheza ina sare tatu ikiwa ni timu yenye sare chache

    ReplyDelete
    Replies
    1. Prison ni bingwa wa sare lakini simba ni mbovu wa sare maana yake yeye anataka ushindi na sio sare

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic