June 25, 2020


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool kwa sasa anasubiri kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kushinda mabao 4-0 mbele ya Crystal Palace kwenye mchezo uliochezwa jana Uwanja wa Anfield bila ya mashabiki kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Liverpool inasubiri kutwaa taji hilo ikiwa imepita miaka 30 ikiwa inaongoza kwenye msimamo ikiwa na pointi 86 kibindoni baada ya kucheza mechi 31 ikishinda mbele ya Manchester City, Julai 2 itatangazwa rasmi kuwa mabingwa.

Mabao ya Liverpool yalijazwa kimiani na Trent Alexander-Arnold dk 23,Mohamed Salah dk 44,Fabinho dk 55 na Sadio Mane dk 69.


Klopp amesema kuwa kwa sasa wanahitaji pointi mbili ili kufikia malengo yao na timu inapambana kwa kuwa inashirikiana vizuri.

Crystal Palace ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo na pointi zake 42 ikiwa imecheza mechi 31.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic