INAELEZWA kuwa iwapo Simba itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 wachezaji wataogelea mamilioni ya fedha.
Mamilioni hayo watapewa kutoka kwenye fedha watakazopewa za zawadi ya kutwaa ubingwa huo ambapo itakuwa ni mara ya tatu mfululizo.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na poini 78 baada ya kucheza mechi 31 inasaka pointi mbili ili kutanagzwa kuwa bingwa ambapo Jumapili itamenyana na Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine.
Mchanganuo wao upo namna hii :-Zawadi ya ubingwa wa ligi Kuu Tanzania Bara (Milioni 87) watapewa wachezaji na viongozi wa bechi la ufundi kugawana.
Mwenyekiti wa Bodi, Mohamed Dewji atatoa milioni 200 kwa wachezaji na viongozi wa bechi la Ufundi kama zawadi yake kwa kutwaa ubingwa wa ligi.
Fedha Zingine ambazo wachezaji wa Simba watapata ni milioni 100 kutoka Sportpesa ikiwa ni matakwa ya kimkataba.
Fetty Dewji kupitia udhamini wa Mo Energy na Mo Halisi watatoa zawadi ya Milioni 75. wadhamini wa kutengeneza Jezi za Klabu ya Simba Kampuni ya Uhlsport wao watatoa milioni 50 Kama zawadi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara (2019/20).
Fedha hizo zote Bodi imedhamiria wapewe wachezaji na viongozi wa bechi la Ufundi.
Hesabu inakuwa jumla Milioni 512. Wachezaji wa Simba 29 viongozi wa bechi la Ufundi 11 Jumla 40. Kila mchezaji na Kiongozi wa bechi la Ufundi atapata Milioni 12.8.
Akizungumza na Saleh Jembe, Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe, amesema kuwa mpango wa kuwapa zawadi wachezaji utatolewa taarifa kamili hivi karibuni.
"Kwa sasa bado hatujakamilisha shughuli nyingine za mechi zetu, kuhusu zawadi ni mpaka pale ambapo tutakubaliana na kuona namna gani tunaweza kufanya ila kwa sasa mambo bado," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment