June 21, 2020


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Azam FC watapambana kuibuka ña ushindi kwa kuwa mchezo uliopita walifungwa bao 1-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya.


"Kila kitu kipo sawa na tutakamilisha ushindi kwa kucheza mpira wa pasi na kutulia, tunakumbuka kwamba mchezo wa kwanza walitufunga ila kwa sasa hatutakubali kufungwa tena.

"Mashabiki wajitokeze kutupa sapoti ili kuona namna gani timu itapata matokeo kwenye mchezo wetu mgumu," amesema.

Yanga itamenyana na Azam FC,  Uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic