June 27, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anahitaji kupata ushindi mapema kwenye mchezo wake wa leo dhidi ya Ndanda FC utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa kosa kubwa walilofanya kwenye mechi yao dhidi ya Namungo ni kushindwa kumaliza mchezo kipindi cha kwanza jambo lililowafanya wakatoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

“Mechi zetu zinazofuata hatutakubali kuona kwamba tunamaliza kipindi cha kwanza tukiwa hatujapata bao, nimewaambia wachezaji wangu na tumekuwa tukifanyia kazi makosa yetu hivyo wapinzani wetu wajipange, tunahitaji pointi tatu.
“Kikubwa kilichopo mbele yetu kwa sasa ni kuona namna gani tunamaliza mechi zote zilizobaki kwa kupata ushindi hakuna kingine ambacho tunakifikiria, tunahitaji kumaliza tukiwa nafasi ya pili haitawezekana iwapo hatutashinda mechi zetu zilizobaki,” amesema Eymael.
Mchezo wa kwanza Yanga ilishinda bao 1-0 Uwanja wa Nangwanda Sijaona, ikiwa nafasi ya tatu na pointi 57 inakutana na Ndanda iliyo nafasi ya 15 na pointi 35 zote zimecheza mechi 31.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic