June 27, 2020


UONGOZI wa Biashara United umesema kuwa utalipa kisasi cha kufungwa mabao 2-1 na Azam FC kwenye mchezo wao wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Chamazi kwa kuwa wameingia anga zao.
Biashara United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuinyoosha mabao 4-0 KMC, Uwanja wa Karume.

Nyota wake Atupele Green alisepa na mpira jumla baada ya kufunga mabao matatu kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Karume.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mwenyekiti wa Biashara United, Seleman Mataso amesema kuwa wamejipanga kupata pointi tatu mbele ya Azam FC kwa kuwa wameingia anga zao.
“Tusema kwamba wapo anga zetu kwa sasa na hesabu kubwa ambazo tunazo ni kuona timu inamalizia ikiwa nafasi tano za juu, njia pekee itakayotupeleka hapo ni kupata ushindi hakuna jambo jingine.
“Mchezo wetu wa kwanza tulifungwa hivyo ni wakati wetu mzuri kulipa kisasi, wachezaji na benchi la ufundi lipo tayari kuona tunabakiza pointi tatu nyumbani,” amesema Mataso.
Biashara United ipo nafasi ya tisa ikiwa na pointi 44 huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili na pointi 58 zote zikiwa zimecheza mechi 31.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic