TIMU ya Aston Villa inazidi kupoteza matumaini ya kubaki ndani ya Ligi Kuu England msimu ujao baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa mabingwa Liverpool.
Sadio Mane, nyota wa Liverpool alifungua pazia la kucheka na nyavu dakika ya 70 na msumari wa mwisho ulipachikwa kimiani na Curtis Jones dakika ya 89 kwa pasi ya kichwa ya Mohamed Salah.
Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta alitumia dakika 17 kuitumikia Villa, ambapo aliingia dakika ya 73 akichukua nafasi ya Keinan Davis.
Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha jumla ya pointi 89 huku Aston Villa ikiwa nafasi ya 18 na pointi zake 27 ikiwa zote zimecheza mechi 33.
Julai 9, Villa ina kazi ya kumenyana na Manchester United inayonolewa na Ole Gunnar Solskjaer ambayo ipo nafasi ya 5 na pointi 55.
0 COMMENTS:
Post a Comment