LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hana hesabu kuhusu mchezo wake wa Simba wa hatua ya nusu fainali unaotarajiwa kuchezwa Julai 12 Uwanja wa Taifa mpaka amalize mechi zake mbili muhimu.
Jana Yanga ilimalizana na Biashara United kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Karume kwenye mchezo wa ligi uliokuwa na ushindani mkubwa.
Julai 8 ina kibarua mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa michezo yote wanayocheza ni muhimu ila lazima afikirie ya ligi kwanza.
“Kuna mchezo dhidi ya Simba hapo baadaye hilo ninajua ila ni lazima tuanze kujipanga na mechi hizi ambazo zipo mbele yetu ambazo nazo ni ngumu tukimaliza hapa ndipo tutaanza maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Kombe la Shirikisho,” amesema Eymael.
Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 33 inakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya nane na pointi 46.
Mashakili ya Morrison na Shishimbi sasa yanazungusha vichwa. Mlisema Kwanza la muhimu kombe la Shirikisho na mfunge mechi za ligi zote zilizobaki ili muipate nafasi yapili muweze kushiriki za mataifa. Mambo yatibuwa vichwa na mnasema la Shirikisho munalieka kan do mpaka baadae na huku zikibaki siku tano tu. Kama hamtojituliza ndipo mtakapokosa kila kitu.
ReplyDelete