KIKOSI cha Azam FC leo kimefanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa Jumapili, Uwanja wa Samora.
Azam FC iliyo chini ya Aristica Cioaba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Gairo.
Inakutana na Lipuli iliyotoka kushinda mabao 2-0 mbele ya KMC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa uwanja wa Samora.
Leo kikosi cha Azam FC kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu cha Mkwawa (MUSE).
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya ushindani na wana amini watapata matokeo chanya kwenye mchezo huo.
Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 65 inakutana na Lipuli iliyo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 40 zote zikiwa zimecheza mechi 35 za ligi.
Mchezo utakuwa na ushindani kwa kuwa Lipuli inapambania nafasi ya kubaki ndani ya ligi huku Azam FC ikisaka nafasi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment