July 24, 2020

MAUMIVU mengine huwa ni magumu kuyeyuka ndani ya mioyo kutokana na matokeo ambayo unayapata kutokuwa kwenye hesabu mwanzo unavyoanza.
Hakuna ambaye alitarajia leo kungekuwa na mvutano mkubwa kati ya uongozi wa Yanga na mchezaji Bernard Morrison ambaye alianza vizuri ila mwisho ameanza kuboronga.
Katika hili ni muhimu iwe funzo kwa timu nyingine kutazama aina ya wachezaji wakigeni ambao wanaweza kupata nafasi ya kusajiliwa kwenye timu zao.
Kila mmoja anahitaji kupata mchezaji mzuri hasa kwa kuwa wakati ujao ni muda wa usajili na kila timu itakuwa na wakati wa kufanya usajili.
Ni jambo jema kuwaepuka wachezaji aina ya Morrison kwani ni wavurugaji na wakatili ndani na nje ya uwanja licha ya kuwa na uwezo mkubwa.
Awali alianza vizuri na kila mmoja alikuwa anampenda kuanzia mashabiki mpaka wachezaji wenzake kwa sababu alikuwa anatimiza wajibu wake vizuri licha ya kwamba alikuwa na matatizo yake binafsi.
Ninaskia kwamba watani wa Yanga ambao ni Simba wanahitaji saini yake sasa sijajua picha hii itakwishaje ngoja tusubiri na tuone itakuaje maana mambo yanazidi kuwa mengi.
Kikubwa kila mchezaji anahitaji kucheza na anapenda kutimiziwa wajibu wake ikiwa ni pamoja na stahiki zake hili ni jambo la msingi lakini naye pia anapaswa atimize wajibu wake uwanjani.
Morrison amekuwa ni mchezaji ambaye anaonyesha ana utovu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja kwa kuwa ikiwa unatolewa kwenye mchezo na kutokomea kusikojulikana huo sio uungwana na hakuna anayefundishwa kufanya hivyo.
Lakini bado ninarudia kusema kwamba kuna jambo ambalo kiungo huyo mshambuliaji anapaswa kujifunza kupitia jeuri yake huku timu nazo pia zikipaswa kujua aina ya wachezaji ambao wanaletewa na wale ambao hawawatambui.
Kitu cha msingi kabla ya usajili ni muhimu kuwa na maskauti ambao watawafuatilia kwa umakini wachezaji ambao watajiunga na timu kwenye msimu wa usajili.
Hii itasaidia kupunguza sarakasi hizi ambazo zinaendelea kwani kila mmoja anasema analolitambua yeye jambo linalowavurugavuruga mashabiki wakishindwa kujua wakamate lipi waache lipi.
Umuhimu wa kuwachunguza wachezaji tabia zao za ndani na nje ya uwanja zitasaidia kila mchezaji ambaye atasajiliwa ndani ya timu kupambana kutimiza majukumu yake na kuachana na vitendo ambavyo sio vya kiungwana.
Mpira una kanuni zake ambazo zinapaswa zifuatwe na kila mmoja ambaye anaishi maisha ya mpira ikiwa ni pamoja na wachezaji na viongozi.
Hakuna mchezaji ambaye anaweza kupata jina bila kupita kwenye timu ambayo inamfungulia maisha yake ya kujulikana kwa mashabiki pamoja na timu nyingine ambazo zinahitaji saini yake.
Kwa maana hiyo ni kwamba kila mchezaji anapaswa awe na nidhamu kwenye timu yake pamoja na wachezaji wenzake ili aweze kuwa na maisha marefu kwenye soka lake.
Uwezo wa kuupanda mpira hilo halikatazwi lakini uwezo wa kuipanda timu na kudhani kwamba yeye ni mkubwa naona halipo sawa kwani haijawahi kutokea duniani hasa kwenye ulimwengu wa mpira.
Tuachane na masuala ya Morrison ninaamini kwamba kwa ajili yake amekuwa ni darasa kwa wengine katika wakati mwingine wa kufanya maamuzi hasa ya usajili wa wachezaji ambao hawajulikani.
Sasa ninazungumza kuhusu lala salama ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa zimebaki mechi mbili kwa kila timu ili kujua nani atashuka ndani ya ligi ya Bongo.
Tayari Singida United yupo mjini akiwa na tiketi yake mkononi ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza ana uhakika wa kuanza maisha mapya msimu ujao wa 2020/21.
Ana nafasi ya kujipanga kurejea tena ndani ya ligi wakati ujao kwa kuwa alikuwa analeta ushindani ila hakuwa na bahati msimu huu kutokana na kuanza vibaya tangu ligi ikianza.
Kila timu kwa sasa inahaha kusaka ushindi na inapambana kwa hali na mali huku nyingine zikiwa zimeshasahau masuala ya kushuka daraja kwa kuwa zimetimiza malengo yao.
Nimengundua kwamba timu nyingi huwa zinajisahau pale zinapokuwa na mechi nyingi mkononi zinafikiri kwamba zitabaki milele na hizo mechi jambo ambalo sio kweli.
Tazama Ndanda FC ambayo ilianza kwa kusuasua ilikuja kuchangamka mwishoni na sasa inaparangayika kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi msimu ujao.
Hata Singida United nayo imefufuka ghafla kwenye mchezo wake dhidi ya Ruvu Shooting ambayo ipo ndani ya 10 bora kumbe inamaanisha kwamba ilikuwa na uwezo wa kufanya vizuri tangu awali ila haikujua inahitaji nini.
Kwa sasa ikiwa nafasi ya 20 kibindoni ina pointi 18 bado ni chache kwa Singida United ambayo ilianza kwa kasi na mwisho wa siku inapita kama upepo hii ni mbaya.
Wakati mwingine timu zote pale ligi inapoanza zinapswa zijipange haswa kushiriki ligi na kuleta ushindani na sio kusubiri mpaka ligi inakaribia kuisha na zenyewe zinazinduka.

7 COMMENTS:

  1. Morison mmempa kichwa nyi waandishi wa habari mlikuwa hamna habari nyingine zaidi ya kuandika Morison muuaji wa Simba mbona hamumuandiki Fraga, Luis au Chama ushabiki na mapenzi yenu ndio vimemfikisha hapa

    ReplyDelete
  2. Kuanzia tarehe 12/7 na kuendelea wasomaji walitegemea kusoma "Chama, Luis na Kahata ni Izrael wamewatoa roho zao wachezaji wa Yanga" Lakini wapi????????? Hilo halipo humu kwenye hii blog page

    ReplyDelete
  3. mapovu ruksa.nyie acheni zenu ,bado mnafikiria mtafika mbali ngoja zamu yenu.

    ReplyDelete
  4. Upumbavu tu hawa waandishi wa habari,,tatzo lao unafki mwngi,na wao ndo wanaowaharbu wachezaji kwa kuwasifia ujinga wao

    ReplyDelete
  5. Ndugu Mwandishi unatakiwa uwe objective, hapa umekuwa biased sana, sio uandishi huu, uandishi wa namna hii unapaswa kufanywa na mwanachama wa Yanga maana yeye ataandika hiyo article kama shabiki

    ReplyDelete
  6. Ilikuwa habari si habari Muuaji wa simba,Tukikohoa kidogo Muuaji wa simba kafanya hivi,Mara kidogo Muuaji wa simba jamani.Matokeo yake Muuaji wa simba kashindwa kuja kufanya lolote la maana kunako mechi ambayo yanga piga ua walitakiwa kushinda.Na si kushindwa kufanya lolote kwenye mechi ya fainali tu la hasha bali Morrisoni aliivua nguo yanga na benchi lao la ufundi na kuonekana yeye kweli yupo juu zaidi ya timu baada ya kutokomea nje ya uwanja baada ya kocha wake kumfanyia mabadiliko ya kiufundi kwani simba walihakikisha Morrisoni hachezi kwa kiwango anachokitaka na simba walifanikiwa kweli kweli . Kumbuka maelekezo ya Mganga wa Yanga katika mechi ile ilikuwa Yanga lazima watangulie kufunga bao sasa simba ilipopata bao kabla wao kufunga wachezaji wengi wa Yanga kiimani waliishiwa nguvu akiwemo Morrisoni mwenyewe hata wale wa benchi. Labda tujikumbushe uovu wa Yanga katika sajili juu ya simba .Yanga walishawahi kumsajili Mbuyu twitwe aliekuwa mchezaji halali kabisa wa simba waliekwisha malizana nae kimaslahi,Yanaga pia walisha wahi kumsajili Ramadhani kesy akiwa mchezaji halali wa kimkataba wa simba,Yanga pia walimsainisha piusi Buswita wa mbao aliekuwa keshamalizana na simba na kumpatia anachotaka na mchezaji huo kufungiwa kwa kusaini timu mbili msimu mmoja.Bila kusahau Yanga walimrubuni Ramadhan kesy akiwa mchezaji wa simba kuifungisha simba kwenye mechi kati yao na kweli kesy aliwapa Yanga goli na kutoa asisit kadhaa kwa washambuliaji wa yanga ili yanga iifunge simba.Ila haya yote waandishi hawayaoni kama ni mambo mabaya? Morrison aliesainiwa mkataba na viongozi wa Yanga bila ya matakwa yake leo anaonekana mkorofi? Nani mkorofi kati ya Yanga na Morisoni? Hapa muandishi kaandika blah blah kibao za kutunga za kinafiki kuhusu Morrison yaani ni one side story lakini kashindwa kuelezea madhaifu ya Yanga.Na kubwa hasa ya huu ukanjanja wa hii habari hapo juu unakuja kutokana na kuwa Simba wameonesha dhamira ya kutaka kumsajili Morrisson. Kumbuka ni jana tu Mwakalibela kaonekana kwenye mitandao ya kijamii akilia kama kinda la ndege kwa kutendewa maovu ndani ya yanga sasa akilia Morrison anaonekana mkorofi? Sasa wenye masikio wasikie na wenye macho watazame na wenye mdomo waseme kuwa tuwache unafiki Morrisson sio tatizo,tatizo ni Yanga na ni wao ndio waliomtengenezea mazingira yakuwa Morrison huyu wa sasa. Na kama simba wana nia kweli ya kumsajili na uwezekano huo upo basi wasisite wafanye haraka kumsajili kwani Azam nao wapo mbioni kukamilisha sajili yake.

    ReplyDelete
  7. Mirrison ameukana mkataba mbele ya TFF kuwa mkataba wa miaka 2 hajausaini badala yake viongozi wa Yanga wameghushi saini yake, mpaka muda huu TFF wameomba msaada kwenye vyombo vya dola vinavyoshughulikia makosa ya jinai kuchunguza saini iliyopo ndani ya mkataba. Mbona hili halijaandikwa humu? Morrison anaendaje kambini kwa sasa wakti mkataba uliisha tarehe 14/7/2020?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic