July 22, 2020


LEO Yanga inatupa kete ya 37 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo watamenyana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro majira ya saa 10:00 jioni.

Wachezaji wao nane wataukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali ambazi zimeelezwa ikiwa ni pamoja  na wale ambao ni majeruhi pamoja na wale ambao hawapo kwenye mpango wa kocha.

Nyota hao ni pamoja na:-Haruna Niyonzima anasumbuliwa na majeraha ya goti, Mapinduzi Balama yeye pia anasumbuliwa na majeraha aliyopata mazoezini, Papy Tshishimbi bado hajawa fiti.

Ally Ally, Andrew Vincent, Eric Kabamba, Ramadhan Kabwili, Raphael Daud hawa hawapo kwenye mpango wa mwalimu, Luc Eymael hivyo iwapo atawatumia ni kwa muda mchache ndani ya kikosi cha leo.

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 68 inamenyana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 41 zote zimecheza mechi 36.

3 COMMENTS:

  1. Inaonesha Morrison yumo ndani ya kikosi kitachokikabili Mtibwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. MCHUKUENI HUYO MORISSON KAMA MLIVYOMCHUKUA NIYONZIMA, GADIEL,AJIBU NA KAKOLANYA
      MATOKEO YAKE MNAYAJUA AU SIO!!!! YANGA TUMESHAAPA HATUTOCHUKUA WACHEZAJI WA SIMBA HATA MKITUPA BUREEEEE

      Delete
  2. Na wala sio sahihi kusema akina Kabwili, Ally Ally, kabamba, Andrew Vicent na Rafael Daudi ambao mwalimu kasema hana mpango nao wewe mwandishi unasemaje kuwa ni wa kikosi cha kwanza? Hapo wa kikosi cha kwanza ni Niyonzima na Tshishimbi tuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic