July 17, 2020


KOCHA mkuu wa AS Vita ya Congo,Florent Ibenge amesema kuwa anaweza kuwa kocha wa Simba endapo tu timu hiyo itakuwa inamuhitaji na itafanikiwa kupata saini yake.

Hivi karibu kumekuwa na taarifa mbalimbali zikimuhusisha kocha huyo kutakiwa na Simba kwaajili ya kuchukuwa nafasi ya kocha wa sasa wa Simba, Sven Vandenbroeck.

Akizungumzia juu ya kuhitajika na Simba, kocha Ibenge amesema kuwa kwa sasa bado ni tetesi na asingependa kuongelea tetesi huku akifunguka kuwa kama timu hiyo inamuhitaji basi yeye hana shida kwani kinachotakiwa ni Simba kufuata taratibu za usajili.

"Mimi ni kocha mkubwa nisingependa kuongea kuhusu tetesi zinazonihusu mimi kuhitajiwa na Simba,kuifundisha timu hiyo inawezekana lakini kama wao wananihitaji wanatakiwa kufuata taratibu zote za usajili.

"Simba ni timu nzuri katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati nakumbuka ilitufunga kwenye ligi ya Mabingwa Afrika, naamini wanamipango ya kufika mbali,"alisema Kocha huyo.

4 COMMENTS:

  1. Huyu anaweza kuipeleka mbali simba

    ReplyDelete
  2. Hizo habari zinatengenezwa ili usome au kununua magazeti yao

    ReplyDelete
  3. Haliingii akilini aliyoyafanya Sven abadilishwe slete mwengine na Kuna usemi "kama hunijui, jaribu mwengine"

    ReplyDelete
  4. kinachomta pengine ni mkataba, mkataba wa sven ni mwaka mmoja wacha wenyewe wafanye tusiwaingilie mamlaka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic