July 27, 2020


LUC Eymael aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa yeye sio mbaguzi ingekuwa hivyo asingeweza kufanya kazi ndani ya bara la Afrika kwa miaka mingi.

Leo, Eymael ametimuliwa kazi na mabosi wake Yanga kutokana na kitendo chake cha kutoa lugha zisizo za kiungwana zenye viashiria vya ubaguzi wa rangi kwa mashabiki wa Yanga kupitia sauti yake kwa vyombo vtya habari.

Kauli aliyoisema Eymael kuhusu mashabiki ni hii hapa:-"Sifurahii nchi hii (Tanzania). Nyinyi ni watu ambao hamjaelimika. Nimechukizwa. Sina gari, WiFi au DSTV. Mashabiki hawajui chochote kuhusu soka. Ni kama nyani au mbwa wanavyopiga kelele."

Kuhusu ubaguzi wa rangi Eymael amesema:"Kama ningekuwa mimi ni mbaguzi wa rangi basi nisingeweza kufanya kazi miaka mingi Afrika, pia nisingeweka ishara ya kupinga ubaguzi na ndio maana jana nilipiga goti moja pale uwanjani,".

4 COMMENTS:

  1. Huyu aondoke haraka. Dhatau zimepitiliza. Kama Tanzania haifai kafuata nini huku. Tutajuaje pengine hata uuko alukotoka ndio zake ila labda walikuwa wanamvumilia tuu, huyu kazidi mpaka. Afukuzwe na aslipwe chochote, maana nyani au mbwa hana uwezo wa kumlipa binadamu mshahara

    ReplyDelete
  2. Halafu huko kwao ubelgiji kuna nini cha maana,he is so dumb and stupid,kashindwa maisha kwao ndio maana kaja africa,ana akili ya kimasikini sana yaani mshahara analipwa anashindwa kaweka dstv na wifi,basi aolewe awekewe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic