July 27, 2020



BEKI wa kati wa Simba, Pascal Wawa, anatarajiwa kuwepo kwenye sehemu ya kikosi kitakachoivaa Namungo FC katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho, maarufu kama FA.

Wawa, Julai 16 alionyeshwa kadi mbili za njano kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu na kutolewa nje katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ulikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu bila kufungana ndani ya dakika 90.

Fainali ya FA inatarajiwa kujaa upinzani mkubwa, imepangwa kupigwa Agosti 2, mwaka huu Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu Bara, kifungu cha 38 kifungu kidogo cha kwanza: “Mchezaji atakayetolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kadi mbili za njano (second yellow card) katika mchezo wa ligi, hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuata wa timu yake.”

Hivyo, mchezo uliofuata wa Simba ulikuwa jana Jumapili, Julai 27 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika, Moshi na beki huyo hakucheza mchezo ule.

Wawa anatarajiwa kuwa huru katika mchezo unaofuata wa fainali hiyo ya FA kama Kocha Mkuu wa timu hiyo MbelgijiSven Vandenbroeck, akihitaji kumtumia watakapocheza dhidi ya Namungo.

Kocha Msaidizi wa SimbaSeleman Matola, alithibitisha hilo kwa kusema: “Kanuni zipo wazi, Wawa atakuwepo sehemu ya kikosi chetu kitakapocheza fainali ya FA, ni baada ya kumaliza adhabu yake ya kadi nyekundu.”

2 COMMENTS:

  1. Muandishi mbona unapotisha. Unasema dakika 90 zimemalizika Bila ya kufunga a ilhali Simba iliishinda 2 na Costal 1

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lin hyo Simba ilifunga mbili au ww umeshindwa ku elewa sio polisi ni costal Union ya Tanga na kule moshi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic