July 31, 2020


UONGOZI wa Simba umetangaza kuwa wachezaji watakaobaki kuendelea kuvaa jezi za timu hiyo msimu ujao ni wale walioonyesha ubora mkubwa msimu huu wa 2019/2020.

Kwa maana hiyo, wachezaji ambao huenda Simba ikaachana nao kutokana na kutotoa mchango mkubwa katika timu hiyo ni Yusuph Mlipili, Tairone do Santos, Rashid Juma, Haruna Shamte na Sharraf Eldin Shiboub.

Wakati timu hiyo ikipanga kutembeza panga hilo, tayari wapo wachezaji wanaohusishwa kujiunga na timu hiyo kwa msimu ujao ambao ni Michael Sarpong, Bernard Morrison na Bakari Mwamnyeto.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alisema kuwa soka siyo mchezo wa kujificha, wale wachezaji walioonyesha na wasioonyesha ubora wao wameonekana, hivyo benchi la ufundi na uongozi hawatatumia nguvu kuwaondoa kikosini walioshindwa kuendana na kasi ya timu.

Senzo alisema kuwa kazi ngumu ipo kwenye usajili wa wachezaji pekee kwa kutumia ripoti ya kocha wao Mbelgiji, Sven Vandenbroeck ili kuhakikisha wanawapata nyota wanaostahili kuichezea Simba msimu ujao.

Aliongeza kuwa, zipo baadhi ya nafasi zinazohitaji kufanyiwa maboresho kwa kuwasajili wachezaji bila ya kufuata ripoti ya kocha ambazo ni ushambuliaji na safu ya ulinzi ya kati inayoongozwa na Erasto Nyoni, Pascal Wawa na Kenedy Juma.

“Lipo wazi kabisa, wachezaji tutakaobaki nao msimu ujao ni wale walioonyesha ubora msimu huu ambao tayari umemalizika.

“Kikubwa tutakachoangalia ni mchango upi ameutoa mchezaji, hivyo baada ya hapo ndiyo zoezi hilo la kuwatangaza wachezaji wa kuwaacha litaanza kwani ni lazima tuwaache ili wengine wapya waje kuchukua nafasi zao msimu ujao.

“Tumepanga kufanya usajili wenye tija katika timu, lengo ni kuwa na kikosi imara kitakachotupa ubingwa wa ligi, Kombe la FA pia kufika mbali katika michuano ya kimataifa tutakayoshiriki msimu ujao,” alisema Senzo.

6 COMMENTS:

  1. Kama mchezaji hakupewa nafasi ya kuonesha ubora wake uwanjani wataujuaje kama huyo mchezaji ni bora au la? Wapo wachezaji ambao Sven na Matola waliwakuta kwenye kiwango bora kabisa e.g. Rashid Juma pamoja na umri wake wa miaka 21 alicheza na Al Haly AS Vita lakini wao wamemuweka benchi msimu wote tangu aondoke Uchebe. Its not kwa sasa kusema hakuwa bora. Wanadumaza vipaji vya kesho makocha hawa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli hata pale simba ilipojihakikishia ubingwa bado wachezaji kama Rashid Juma, Shibob, Kichuya hawakupewa nafasi ya kutosha badala yake tuliona ni walewale wa kila siku hata Kakolanya alibaniwa kucheza

      Delete
  2. Kakolanya amecheza mechi na Ndanda, Namungo na Polisi. Rashid Juma amepata bahati mbaya ya kuwa majeruhi muda mrefu na aliporudi hakuwa kwenye kiwango cha kuridhisha.Kichuya alipewa nafasi aka flop. Luis amepunguza sans nafasi ya Rashid Juma.Rashid Juma atapelekwa kwa mkopo Polisi Tanzania. Mlipili yupo na timu Sumbawanga.Hsta hixi ni rumours hakuna uamuzi wa uhakika. Tuache judgement.Tuamini uamuzi wa kitaalamu kwani wao ndio wapo na wachezaji kila siku.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sawa Unknowmn subira yavuta heri ila lisemwalo lipo kama halipo "liko ku mbarabara".

      Delete
  3. Huyu mchambuzi sio wa kumwamini subirini taarifa rasmi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic