INAELEZWA kuwa Simba imeamua kuvuruga mipango ya Yanga kwa kuipata saini ya straika wa Namungo FC, Reliants Lusajo baada ya kuzunguka upande wa pili wa mchezaji huyo.
Simba wameamua kumchukua Lusajo wakitaka straika huyo kwenda kuboresha safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa msimu huu inaundwa na John Bocco na Meddie Kagere.
Lusajo ndiye mchezaji mzawa wa pili kwa kufunga mabao mengi msimu huu ikiwa hadi sasa amefunga mabao 12 katika Ligi Kuu Bara.
Simba ni mabingwa wa ligi hiyo wakiwa na tiketi mkononi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wameshaweka wazi kuwa watahitaji kuongeza nguvu kwenye safu hiyo na mchezaji mzawa ni mmoja wa sehemu hiyo ya mipango.
Habari zinaeleza kuwa, baada ya uongozi wa Simba kukaa katika kikao cha kujadili maboresho katika safu hiyo ya ushambuliaji, kuridhia kwa pamoja kuhakikisha wanainasa saini ya Lusajo.
"Yanga walikuwa wakimfuatilia Lusajo ili waboreshe safu yao ya ushambuliaji, ila tayari tumeshawatangulia, maana mchezaji na meneja wake kwa pamoja wanataka kucheza kwenye timu ya mafanikio.
"Hata uongozi wetu pia umeshakubaliana na uwezo wake,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Lusajo, alisema: “Mimi nipo tayari kucheza timu yoyote itakayonihitaji baada ya mkataba wangu kumalizika, ila hiyo ishu ya Simba na Yanga sidili nayo maana meneja wangu alinitaka nimalizie mechi, hivyo mambo yote ya usajili yeye ndiye anayafuatilia zaidi.”
Nawaambia wakimuona Simba anaingia, basi kwa usalam a wao mkae upande apite kabla ya kukupigeni kkikumbo nanyi hamna ubavu wa kumzuwia
ReplyDeleteUjinga wa kuuza habari.Lini Yanga walisema wanamtaka Lusajo?
ReplyDeleteHata wakimtaka wanakuwa na hakimiliki ya kuzuia timu zingine?
Wanaingiliwa kwa vipi?