July 31, 2020


OLIVIER Giroud, nyota wa Klabu ya Chelsea inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kuondoka ndani ya kikosi hicho na kuibukia ndani ya Inter Milan inayoshiriki Serie A, nchini Italia.
Kocha Mkuu wa Inter Milan, Antonio Conte ambaye alikuwa ni kocha wa Chelsea inaelezwa kuwa amevutiwa na nyota huyo jambo ambalo limeongeza nafasi ya nyota huyo kuondoka ndani ya Chelsea kwa sasa.
Frank Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea bado hajawa tayari kumruhusu mshambuliaji huyo aondoke kwa kuwa bado anaamini ana nafasi ndani ya kikosi hicho cha Chelsea kwa sasa na amekuwa na ushirikiano mkubwa na wachezaji wenzake.
Kesho, Agosti Mosi, Chelsea ina kazi ya kumenyana na Chelsea kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Arsenal na Giroud anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza Uwanja wa Wembely.  
Nyota huyo mwenye miaka 33 raia wa Ufaransa amekuwa kwenye ubora wake chini ya Lampard, kesho anakutana na Arsenal ambao walikuwa ni mabosi wake wa zamani kwenye fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic