July 23, 2020



LEO ndani ya Ligi Kuu Bara,  Julai 23 mambo yapo namba hii:-
Azam FC v Mbeya City, Uwanja wa Azam Complex.

Azam FC ipo nafasi ya tatu  kibindoni ina pointi 66 ina uhakika wa kubaki ndani ya ligi huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 15 na pointi 42 haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi na zote zimebakiwa na mechi mbili.

Lipuli FC v Ruvu Shooting, Uwanja wa Samora.

Lipuli ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 41 na Ruvu ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 47 zote hazina uhakika wa kubaki ndani ya ligi, Ruvu inahitaji pointi moja kujihakikishia nafasi ya kubaki msimu ujao.

Polisi Tanzania v JKT Tanzania,  Ushirika.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya tano na pointi zake 54 ina uhakika wa kubaki msimu ujao sawa na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 8 na pointi 50 zote zimecheza mechi 36.

Coastal Union v Simba, Mkwakwani

Coastal Union ipo nafasi ya saba na pointi zake 52 ina uhakika wa kubaki ndani ya ligi sawa na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 84.

Alliance v Ndanda FC,  Uwanja wa Nyamagana.
Alliance ipo nafasi ya 18 na pointi zake 41 inakutana na Ndanda iliyo nafasi ya 19 na pointi 40, hakuna yenye uhakika wa kubaki ndani ya ligi hivyo utakuwa mchezo mzuri na wenye ushindani.

Mechi zote zitapigwa saa 10:00 jioni isipokuwa ile ya Azam FC dhidi ya Mbeya City itapigwa saa 1:00 usiku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic