July 30, 2020


AGOSTI 2, Uwanja wa Nelson Mandela Simba inatarajiwa kuchezwa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kupambania taji hilo muhimu.

Tayari Simba ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara hivyo iwapo watafanikiwa kulitwaa taji hilo watabeba kombe huku nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ikiwa mikononi mwa mshindi wa pili ambaye ni Namungo.

Ikiwa Namungo itashinda, itatwaa taji na kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa meneja wa Simba. Patrick Rweyemamu amesema kuwa kikosi ambacho kilikwenda Tanga kucheza na Coastal Union kisha kikamalizana na Polisi Tanzania kule Moshi ndicho ambacho kinaelekea Sumbawanga.

"Wachezaji wote wapo vizuri na wanaendelea salama, wale ambao tulikuwa nao Moshi na Tanga ndio ambao tupo, " amesema.

Wachezaji ambao walikosa michezo hiyo miwili na inatarajiwa watakosa fainali ni hawa hapa saba ikiwa ni pamoja na:-Ibrahim Ajib, Sharaf Shiboub, Rashid Juma, Haruna Shamte, Shiza Kichuya, Cyprian Kipenye na Tairone Santos.

5 COMMENTS:

  1. Rashid Juma hajapata nafasi kabisa kwenye kikosi cha Sven na Matola zaidi ya mechi chache za kirafiki.

    ReplyDelete
  2. Hawa wajinga sana baada ya ubingwa ilitakiwa wachezaji wengine wapewe nafasi Rashid Juma aliaminiwa na kocha aliyepita mpaka akawa mzuri hivi utajuaje uchezaji wa mtu kama humpi nafasi

    ReplyDelete
  3. Kocha wa Simba nae chizi. Kwanini anauwa kipaji cha dogo aliyewai kucheza na Ally Ahli na kukabwa na watu watatu - watatu.

    ReplyDelete
  4. Kila kocha ana falsafa yake. Lakini hapa kwa Rashid Juma na Mlipili kocha amechemka sana. Timu zote duniani huwa zinakuwa na wachezaji vijana ambao zinawakuza kwa ajili ya kupunguza gharama kwenye usajili au kuwauza miaka ijayo. Kwangu mimi Rashid Juma na Mlipili walipaswa wawe wanapewa dakika 15 mpaka 20 kwenye zile mechi ambazo hazina umuhimu sana na tayari Simba inakuwa imeshashinda kwa tofauti kubwa ya magoli. Lakini wakulaumiwa zaidi ni wasaidizi wa huyo kocha kwani wameshindwa kumuonyesha kocha hata clip za Al Haly VS Simba au Simba VS Al Masry awaone hao vijana walivyouwasha moto. Kiukweli hao vijana wawili ni hazina ya Simba na taifa kwa miaka michache ijayo lakini kwa uzembe unaofanyika sasa Simba ijaandae kuja kuwanunua kwa pesa nyingi sana miaka michache ijayo iwapo watawaacha waondoke.Wakati mwingine huwa najiuliza hata Mwina Kaduguda ambaye ana taaluma ya ukocha haoni kwamba Simba inapoteza dhahabu inaozea kwenye benchi na timu nyingine zitakuja kujiokotea bure kabisa.

    Huyo Rashid Juma ana kila kitu kuanzia kasi, chenga, krosi nzuri na anakaba vizuri lakini mapungufu yake makubwa ni utulivu kwenye umaliziaji basi. Akipata kocha mzuri wa kumrekebisha kwenye ufungaji halafu akawa anapata muda mwingi wa kucheza yaani ni bonge la mshambuliaji hasa akitokea pembeni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uko sahihi mno. Usisahau alivyoingia kiindi cha pili walipocheza na AS Vita akayasukuma mashambulizi mbele kwa kasi y ajabu. Kifupi, Aussems alielewa umuhimu wa vijana pale Simba na Rashid na Mlipili aliwapa fursa ya kuonesha kipaji chao kila ilipobidi kufanya hivyo na vijana hawa walifurahia sana kucheza. Matola kama kocha msaidizi na mzawa pendekeza kwa uongozi (ni sikivu) kama kocha hatawapendekeza vijana hawa watafutiwe timu za kucheza hata kwa mkopo msimu ujao ili walinde vipaji vyao

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic