July 30, 2020

INAELEZWA kuwa Klabu ya Simba imeingia kwenye rada za kuiwinda saini ya Heritier Makambo aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo. 

Makambo aliachana na Yanga msimu wa 2017/18 akiwa ni namba tatu kwa kutupia ambapo wa kwanza alikuwa ni Meddie Kagere wa Simba aliyetupia 23 na Salim Aiyee aliyekuwa Mwadui FC alitupia 18.

Kwa sasa Makambo anakipiga ndani ya Klabu ya Horoya AC ya nchini Guinea alisaini dili la miaka mitatu kuitumikia timu hiyo. 

Habari zinaeleza kuwa tayari uongozi wa Simba umeshaanza kufanya mazungumzo na mabosi wa Horoya ili kupata saini ya nyota huyo mwenye uzoefu wa kucheka na nyavu.

"Msimu ujao Yanga itapata tabu kwani idadi kubwa ya wachezaji wao wanaweza kuonekana wakikipiga ndani ya Simba na mpaka sasa asilimia kubwa kwa Makambo kukipiga Simba msimu ujao.

"Yanga ilishindwa kuvunja mkataba wake kule Horoya AC ila ndani ya Simba kila kitu kimekuwa sawa na bodi imekubali kuingia chimbo kuiwinda saini yake," ilieleza taarifa hiyo. 

Awali taarifa zilieleza kuwa Yanga ilikuwa inaiwinda saini ya nyota huyo ili arejee ndani ya kikosi hicho.

11 COMMENTS:

  1. Makambo ndani ya Simba hatazomewa hata Mara moja hata pindi akikosea na hayo tumeshayaona pale Mkude alipotiwa pasi kwa kukosa akafunga goli na hapana hata aliyeyataja tena kwani huo nd ndio utamadumi wa Mnyama. Nidham imetawala na hata walivokuwa wa tundu hapo nyuma sasa shuari wakichapa kazi

    ReplyDelete
  2. Nyoooooo kweli wewe nimkia hata historia yako huijui kakimya mama

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eti nyoooo yani kauli zako zinaonekana kabisa wewe ndo mama,kama hujui historia basi simba haina tabia ya kuzomea mchezaji hiyo ni tabia ya utoporo F.C nyie si ndo mlikuwa mnazomea MSUVA mpaka akawa analia

      Delete
  3. Simba kama wanataka kushindana kimataifa watafute wachezaji kama kalivyomsajili Chama haya.mambo ya kuangalia mchezaji aliyecheza yanga hayatawafikisha popote

    ReplyDelete
  4. Makambo hana kiwangi cha kuchezea Simba. Kama kule Horoya kwenyewe ambao hawana ubavu wa kuifunga simba anakaa benchi sana je Simba ataweza nini? Alionekana mzuri Yanga sababu pale yanga hakukuwa na wafungaji. Kwa Simba wamechemsha sana tena sana kumtafuta Makambo. Nahisi Simba nao hawana pesa yan kusajili majembe ya maana toka Afrika Magharibi

    ReplyDelete
  5. Hizi habari si za kweli habari za simba sasa hivi kuzipata ni kazi kwa hiyo waandishi wengi wanafoji habari ili wauze magazeti yao

    ReplyDelete
  6. Ni habari za kutunga tu hizi. Simba sasa hivi habari zao mpaka watoe wenyewe. Bado hawajaanza kufanya usajili.

    ReplyDelete
  7. makambo akikaa mbele ya chama na miqssune atafunga mpaka achukie

    ReplyDelete
  8. Hakuna mchezaji hapo tafuteni wachezaji wazuri acheni na huyo

    ReplyDelete
  9. simba inachukua mchezaji wa timu ya taifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic