KIKOSI cha Simba leo kimefanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Shule ya St. Maurus ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.
Simba ipo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na Namungo FC ipo chini ya Kocha Mkuu Hitimana Thiery.
Sven amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na anaamini mchezo utakuwa mgumu licha ya wengi kuipa nafasi timu yake kushinda.
Thiery amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo licha ya wachezaji wake wengi kusumbuliwa na typhoid na Malaria.
Namungo ina tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho kwa kuwa Simba inaiwakilisha nchi Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:
Post a Comment