August 11, 2020


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa umedhamiria kufanya makubwa ndani ya msimu ujao wa 2020/21 ndio maana umeanza kujifua mapema kabla ya ligi kuanza.

Azam FC ipo chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba raia wa Romania imeshaanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao makao makuu ya timu, Chamazi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabiti amesema kuwa wanatambua kwamba walishindwa kufanya vizuri kwa msimu wa 2019/20 kutokana na kushindwa kufikia malengo ambayo waliyojiwekea.

"Tulishindwa kufikia malengo ambayo tulijiwekea msimu uliopita ila kwa sasa tumeanza kazi ya kukiandaa kikosi mapema ili kuwa bora na kuleta ushindani.


"Imani ni kubwa kwamba tutafanya makubwa msimu ujao hasa ukizingatia kwamba tuna wachezaji wazuri ambao tumewasajili na ni bora hatuna matatizo kwamba tutafanya vizuri," amesema.

Miongoni mwa majembe mapya ambayo yamesajiliwa ndani ya Azam FC ni pamoja na Awesu Awesu, Ally Niyonzima, David Kissu.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic