August 11, 2020



INAELEZWA kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Simba, Senzo Mazingisa, Jumatatu jioni Agosti 10, 2020 alikabidhi ofisi na nyaraka za klabu hiyo.


Kuhusu mbadala wake, ‘kigogo’ mmoja wa klabu hiyo amesema; “Kuna kikao kinaendelea leo ambacho wanajadili nani atakaimu kwa wakati huu huku mchakato mwingine wa kutangaza ajira ukifuata hapo baadaye.


“Nafasi ya CEO ni ya kuajiriwa hivyo taratibu zote za ajira zinapaswa kufuatwa, ni lazima kutuliza akili kufanya hivyo, lakini mtu wa kukaimu atapatikana na huenda akatangazwa hata leo hiihii,” amesema.


Imeelezwa kwamba mtu atakayepatikana kukaimu nafasi hiyo kutoka ndani ya kikao hicho hapaswi kutoka kwenye Bodi ya Wakurugenzi  kwa maana kuwa asiwe mjumbe wa bodi hiyo.


 Crescentius Magori ambaye alimkabidhi majukumu Senzo ni miongoni mwa wanaotajwa kukaimu kiti hicho.


Senzo alibwaga manyanga ndani ya Simba, Agosti 9 kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuwa akiskilizwa huku taarifa nyingine zikidai kwamba mkataba wake ulikuwa umeisha.

9 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Hee wee nyani umekurupukia wapi au ndio shibe ya kuvamia matikiti

      Delete
  2. Simba kuweni makini katika maswala nyeti msituletee wasaliti

    ReplyDelete
  3. Kakurupuka usingizi baada ya shibe ya makande.Usituletee ushuzi.

    ReplyDelete
  4. Magori arudi kwenye nafasi yake coz ni mzalendo kwa klabu

    ReplyDelete
  5. Replies
    1. Senzo anashangaa timu imeuzwa pesa hazilipwi! Plan yake ilikuwa akanunue timu nyingine aipeleke pale Msimbazi ili wapenzi wa mikia nao wawe na timu

      Delete
    2. Hee nyani mwingine kakurupuka tena

      Delete
    3. Senzo nimamluki alitaka kuihujumu Simba kachemka karudi kwa waliomtuma

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic