August 3, 2020


UONGOZI wa Yanga umeeleza kuwa umeachana rasmi na nyota wake saba kwenye kikao ambacho kmefanyika leo.

Wachezaji hao ni wale ambao mikataba yao ndani ya Klabu hiyo yenye maskani yake pale Janganwani imefika tamati na hawajaongeza dili jingine.

Hii hapa orodha ya wachezaji ambao wameachwa na Yanga hivyo hawatakuwa ndani ya kikosi kwa msimu wa 2020/21:-Papy Tshishimbi nahodha wa Yanga,  David Molinga mshambulaiji namba moja ambaye ametupia mabao 11 ndani ya kikosi na pasi moja ya baoa.

 Mrisho Ngassa winga aliyekuwa amewaka mwishoni mwa msimu na mchezo wake wa mwisho alihusika kutoa pasi kwa Molinga. Jaffary Mohamed kiraka rasta kichwani ,Tariq Seif.

Andrew Vincent beki mwenye manywele mwengi kichwani na Mohamed Issa maarufu kama Mo Banka.

5 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Haya ndiyo matatizo ya kusoma kichwa cha habari na ku-comment. Unapenda kuchangia, lkn mvivu kusoma habari, matokeo yake unachangia lolote linalokuja kichwani. Falsafa ya hapa kazi tu inahusu hata katika hili

      Delete
  2. Kwa Jafary yanga wamebugi. Lakini ngoja Tuwaachie wataalam wa soka wengine sisi ni mashabiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni mchango wenye madini kichwani. Kwani sisi ni mashabiki, wataalam walioshauri wanajua kiufundi timu ilikwama wapi hadi isifanye vizuri

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic