August 12, 2020

 


MWENYEKITI wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Tanzania iliyo ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Elias Mwanjala amesema kuwa Bernard Morrison ameshinda kesi yake kuhusu mkataba wake dhidi ya timu yake ya Yanga.

Kamati imeeleza kuwa kulikuwa na mapungufu kwenye mkataba wa mchezaji huyo ambapo kuna ukurasa wa saini umekutwa umekatwa na tarehe zikiwa zimepishana.

 Pia amesema kuwa tofauti kwenye tarehe ndani ya mkataba huo  ni kwamba ipo moja inaonyesha kuwa alisaini tarehe  20 mwezi wa tatu na nyingine inaonyesha tarehe tofauti jambo ambalo limempa ushindi Morrison.

Ameongeza kuwa ilichukua muda mrefu kwa kuwa kesi ilikuwa inahitaji umakini huku akizitaka timu kuwa makini kwenye masuala ya mikataba kwa kuwa wamepoteza muda mrefu kwa jambo ambalo halikuwa na ulazima kutokea iwapo kungekuwa na umakini.


"Tumepoteza muda mwingi kwa ajili ya suala hili, ninadhani ingekuwa maamuzi yangu binafsi ningechukua uamuzi tofauti kabisa katika suala hili ila kwa kuwa kazi yetu tumemaliza basi mchezaji atakuwa huru kuchagua wapi anakwenda.


"Kuhusu kesi yake na mkataba wake wa pili hilo halikuwa chini yetu sisi tulikuwa tunakiliza shauri la mkataba wa kwanza jambo la yeye kusaini sehemu nyingine hilo ni kosa mchezaji mwenyewe amekiri.

"Kwa kufanya hivyo anapelekwa Kamati ya Maadili na haina uhusiano na kesi ambayo tulikuwa tunaisikiliza sisi, yeye ni mchezaji huru kwa kuwa ameshinda," amesema.


19 COMMENTS:

  1. Eymael hakukosea kuhusu umbumbumbu! Badilikeni kumekuwa na dhuruma za kila aina kwa wachezaji.Alishangiliwa kutembelea juu ya mpira na sasa anatembelea juu ya vichwa vyenu! kwa wengine ushindi huu ni zaidi ya 4G kwa sababu wameaibishwa na kudhalilishwa..loh aibu kuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama ameshinda juu ya mkataba wake basi yeye ni mhamiaji halamu kwa sababu amesha kaa nchini kwa zaidi ya miezisita.kibalichake cha kazi kinasomaje?

      Delete
  2. Tuliwaambia Yanga, hawana watu makini kwenye usajili,hili litakuwa fundishooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kweli! Tuangalie work permit yake inasomaje ?

      Delete
    2. Hata kwenye kadi zenu si zimeandikwa bishana mpaka mwisho kwa hiyo hatushangai

      Delete
  3. HIli suala linatakiwa liende mbali zaidi, Vyombo vya dola viwachukulie hatua walioguushi mkataba ili iwe fundisho.

    ReplyDelete
  4. SimbA wangekua makini wange muachia C.E.O aende wabakie na Morrison? Mchezaji anaeongoza kwa utovu wa Nidhamu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba wako sawa kabisa..na lengo la kumchukua Morrison ni kuwadhalilisha Yanga.Siku Morrison kasaini Simba nao Yanga wakatoa tamko la kuwachukulia hatua kali Simna.Mkwara. Acha wamchukue Senzo..Kama wanashindwa kusajili kihalali kukwepa kulipa wachezaji...je wana hela ya kumlipa Senzo? Bado Lwandamina, Plujim na Zahera wanadai

      Delete
  5. utopolo, manyani fc , wa kubwekabweka wazee wa forgery leo wameumbuka washukuru hukumu imeishia hapo walitakiwe washitakiwe

    ReplyDelete
  6. tuache kubadili topiki kuu. tunatoka kwenye dhuruma kwenye mkataba wa Yanga tunaenda kwenye uhalali wake kuendelea kukaa nchini..hivi work permit na kesi ya morrison kudai haki vinahusiana kivipi?

    ReplyDelete
  7. C.E.0 amemaliza mkataba ndiyo maana ameondoka. Alitaka pesa za ziada Simbs wakamgomea .Morrison angekuwa sio muhimu mngemuacha.Nahisi ni povu tu.Pole.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata CEO hawezi kuanza kufanya kazi hadi apate work permit ambayo inabidi Yanga waombe wizara ya kazi.Itabidi wazungumze na Simba kama kibali hicho bado kiko valid na Simba ili wacancell na kukirudisha wizarani.Nchi zingine inabidi kwanza itangazwe hiyo kazi ya CEO na kama wizara wakiridhika hakuna mwenye sifa hizo basi wanaridhia kutoa kibali.

      Delete
  8. Morrison mwanamme wa kweli. Chali + 4G

    ReplyDelete
  9. Keshasema Simba ataiheshimu kwa kila Aina ya heshima. Tume ramba dume la kazi na wache waendelee kulisifu bao lake dhidi ya Mnyama

    ReplyDelete
  10. Kama ningekuwa nina maamuzi ndani ya Yanga ningemuacha aende zake siku ile ile aliyosaini Simba maana ilitosha kudhihirisha kuwa alikuwa anatumika kuihujumu timu.Ikumbukwe kuwa yeye mwenyewe alikiri hadharani kuwa alipokea pesa toka kwa viongozi wa Simba....maana yake alikuwa anakula rushwa kuihujumu timu na kupandikiza migogoro

    ReplyDelete
  11. work permit ni kibali cha kufanya kazi...Work permit na mgeni kuendelea kuwa nchini vi vitu viwili tofauti..Work permit inaweza kuwa imekwisha leo lakini bado mtu ana viza ya kuendelea kukaa nchini..sawa manyani fc...ongezeni akili

    ReplyDelete
  12. siss mashabiki hatutaki tuambiwe et hamna adhabu lzm kieleweke kwa aliyegushu

    ReplyDelete
  13. Naipenda Simba lakini na mpenda Tundu lissu Sana lakini Mimi mwwananchi so babaiki na Ufisadi wa Uadirifu

    ReplyDelete
  14. Mbona hamuulizi work permit ya Senzo hamuulizi?Wakati Simba ndio waliomuombea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic