August 12, 2020

 LEO ni siku ya tatu kwa kuendelea kuskilizwa kwa kesi ya kiungo mshambuliaji wa Yanga ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).

Ilianza kusikilizwa Agosti 10 kisha Agosti 11 bila maamuzi na leo ni Agosti 12 ngoma ipo vilevile.

Kesi hiyo inakilizwa na Kamati ya Hadhi za Wachezaji inamhusu Morrison na Yanga. Mchezaji huyo raia wa Ghana anasema kuwa mkataba wake aliosaini ndani ya Yaga ni wa miezi sita huku Yanga wakieleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili.


Agosti 8, mchezaji huyo alitambulishwa na watani wa jadi wa Yanga, Simba licha ya kuwa ana kesi ya mkataba jambo ambalo limeongeza mvutano wa kesi hiyo.


Jana, Agosti 11, kamati iliahidi leo kutoa maamuzi mapema kwa kuwa nyaraka zilikuwa hazijakamilika ila mpaka sasa hakuna maamuzi yaliyotolewa.

Mashabiki wa soka leo wameendelea kujitokeza kwa wingi makao makuu ya TFF, Karume huku Polisi nao wakiweka makazi yao hapo kwa ajili ya kulinda usalama wa mali na nchi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic