August 12, 2020

 

KIUNGO wa Yanga, Bernard Morrison raia wa Ghana leo Agosti 12 ameshinda shauri lake dhidi ya Yanga ambalo lilikuwa ni kuhusu mkanganyiko wa mkataba wake ndani ya klabu hiyo.


Morrison alikuwa akisema kuwa mkataba wake ni wa miezi sita na umekwisha muda wake huku Yanga ikieleza kuwa alisaini dili lingine la miaka miwili.


Baada ya kesi hiyo kuskilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo tangu, Agosti 10,11 na 12 leo shauri limetolewa rasmi makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).


Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Elias Mwanjala, amesema mkataba wa Yanga na Morrison, una mapungufu makubwa upande wa Yanga na wamempa faida Morrison.
.
"Tumekuwa makini katika kufuata haki na kamati yetu ilikuwa makini, kulikuwa na mapungufu makubwa upande wa tarehe ambapo kuna sehemu ilionyesha kuwa amesaini Machi 20 na nyingine ikionyesha tarehe tofauti.

"Pia kuna ukurasa wa saini kwenye mkataba unaonyesha kuwa umekatwa jambo ambalo linaonyesha kwama kulikuwa kuna tatizo kwenye masuala ya mkataba ni mapungufu makubwa hivyo tunampa ushindi Morrison anakuwa huru kwa sasa.

"Kazi yetu tumemaliza ila Morrison anapelekwa kamati ya Maadili ya TFF kutokana na kosa la kusaini mkataba na timu nyingine (Simba), wakati kesi yake inaendelea kusikilizwa na kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji...

"Kesi hii inayokwenda kamati ya maadili, haina mahusiano na hii ya Yanga dhidi ya Morrison, ambayo yeye ameshinda na ni mchezaji huru. Mchezaji mwenyewe amekiri kuwa amefanya hivyo, ikiwa Yanga hawajaridhika na maamuzi haya ni ruksa kwenda kukata rufaa," amesema.

.

11 COMMENTS:

  1. Nawashauri yanga wakubali yaishe tuu. Wakienda FIFA nawahakikishia watatelemshwa daraja. Hapa kidogo uingwana umetumika kule hakuna kupinda sheria wallah.

    ReplyDelete
  2. Hili suala kama lingeenda mahakamani nina hakika yangefichuka mengi sana kwa pande zote nne;yaani Yanga,Morrison,Simba na TFF lakini kwa sababu lilikuwa linaendeshwa na kuamuliwa na pande moja ambayo nayo inahusika na ubabaishaji wameona wajivue lawama kimtindo.Tujiulize ilikuwaje huyu mchezaji alicheza ligi na FA C up ilhali hakuwa na mkataba na klabu yake?alipataje leseni?kanuni mojawapo ya usajili ni lazima mkataba wa mchezaji usajiliwe TFF ili mchezaji apewe leseni,sasa cha kujiuliza alipataje leseni kama hakuwa na mkataba ukizingatia ni mchezaji wa kigeni?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkataba unaosemwa hapa unaanzia msimu mpya na si ulioisha mkubwa

      Delete
  3. Awali ulikuwa sawa mkataba wa miezi sita uliisha July, tatizo ni extension ile ya miaka miwili

    ReplyDelete
  4. Uungwana ni Yanga kukubali yaishe maisha yaendelee maana mchezaji mwenyewe ameshaamua kuachana na klabu sasa kuna haja gani ya kumng'ang'ania mwisho wa siku atakuwa corona sugu tu ndani ya timu maana tayari alishasambaza sumu na kuleta mgawanyiko miongoni mwa wachezaji.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio mchezaji ameamua kuachana na yanga ishu ni kwamba yanga wamefoji mkataba

      Delete
    2. Ngoja tusikie Yanga nao wanasemaje...maana mkataba mpya alilipwa dola elfu 25. Alilipwa vipi wakati hakujaza mkataba mpya yeye???..hapa Kuna magumashi tu hakun lolote kwenye hilo l maamuzi

      Delete
  5. Yanga jamani Dunia itatushangaa. Achaneni na huyo. Hivi angekuwa mchezaji mkubwa angekaa bila timu mwaka mzima hadi akaokotwa na Eymel. Huko Ghana ata timu ya Taifa hatujawahi kumsikia. Mnatuaibisha wenzenu tunaokaa nje. Yani watu wanakaa siku mbili wanaacha kazi zao kumjadili huyo mtu. Mwisho wa siku watu wanatushangaa. Sasa ndio naelewa kwa nini ata vitimu vya Burundi/Msumbiji kwa wamakonde tunavishindwa

    ReplyDelete
  6. Wewe sio kirahisi hivyo. Watu wamechana mpaka saini ili wafanye forgery. Wathubutu kukata rufaa CAS kama hawajateremshwa daraja na kufungiwa kusajili. Nkana wamefungiwa kusajili kwa kushindwa kumlipa mishahara mchezaji. Hapa Yanga wamelindwa wakate rufaa waone moto.

    ReplyDelete
  7. Utopolo mmedoda, Hamna uelewa na mpira msije mkajifunga CAS mkaongezewa adhabu shauri yenu. Kubalini matokeo tunawapenda. Viongozi wenu Ni vivuli hawajui Nini maana ya mpira mpaka wanaiingiza klabu choo Cha like * tuliieni msije tukawapoteza kwenye soka*

    ReplyDelete
  8. Yaani viongozi wa yanga wananipa wasiwasi sna yaan hapa umefanyiwa ungwana unataka kwenda fifa? aisee daaah wajaribu waone

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic