August 4, 2020


CHELSEA iliyo chini ya Kocha Mkuu, Frank Lampard inaelezwa kuwa imepania kufanya maboresho makubwa msimu ujao kwa kuwaweka sokoni nyota wake wanne ili ipate fedha kukamilisha usajili wa nyota wapya ndani ya kikosi hicho.
Chelsea bado ina mamivu ya kupoteza taji la FA mbele ya Arsenal kwa kufungwa mabao 2-1 iliyochezwa Uwanja wa Wembley huku wakimaliza Ligi Kuu England wakiwa nafasi ya nne.

Wachezaji wanaotajwa kuwekwa sokoni wote ni mabeki ni pamoja na Kurt Zouma, Andreas Christensen, Emerson Palmieri na Marcos Alonso wamewekwa sokoni.

 Lampard inaelezwa kuwa kwa sasa anapambana kuona namna gani anaweza kubaki na  N'Golo Kante anayecheza nafasi ya kiungo yeye anahitaji kuondoka kwenye kikosi hicho.
Zouma mwenye miaka 25 na Christensen mwenye miaka 24 wapo kwenye mchakato wa kuuzwa ili kuipa timu hiyo mkwanja wa kutosha kwa ajili ya kukamilisha usajili kwa wachezaji wengine vijana ambao Lampard anawahitaji.

1 COMMENTS:

  1. sijawahi kuona kocha wa kiingereza huyu ni boya kabisa angalia wachezaji anawauza hayupo hata mmoja wa kiingereza, ubaguzi tu timu imejaa waingereza tupu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic