August 4, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa sababu kubwa ya kuachana na nyota wao Papy Tshishimbi ambaye ni nahodha wa kikosi hicho ni kushindwa kufikiana makubaliano kwa pande zote mbili.

Tshishimbi mkataba wake unamalizika rasmi Agosti 12 kwa mujibu wa kaimu katibu, Simon Patrick ambapo atakuwa huru kusepa ndani ya kikosi hicho baada ya jana, Agosti kuwa miongoni mwa nyota walioachwa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wameachana na Tshishimbi kwa kushindwana pande zote mbili kuelewana.

"Hakuwa ni mpango wote kuachana naye jumla lakini kilichotokea ni kwamba wote tumeshindwa kuelewana hasa kwa upande wa makubaliano.

"Sisi tunachokifanya ni kuskiliza namna mchezaji anavyosema nasi pia tunaweka masharti yetu pale ambapo inashindikana inasababisha tunaachana na mchezaji," amesema Bumbuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic