August 19, 2020

 
OFISA Habari wa Simba, Haji Manara leo Agosti 19, 2020 amefuta kauli yake ya kustaafu nafasi yake ya ndani ya Klabu ya Simba.

Agosti 16, Manara alisema kuwa anampango wa kuachia ngazi kwenye masuala ya uongozi ndani ya Simba kwa kuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiafya lakini angebaki kuwa mshauri na muhamasishaji wa Klabu ya Simba kwa kuwa ni mwanachama.

Leo, Agosti 19 Manara amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuondoka ndani ya Simba kwa kuwa amethibitishiwa na wataalamu wa afya kuwa yupo fiti.

"Jana Agosti 18, nimepimwa na madaktari na wameniambia kuwa nipo fiti, kuanzia kwenye moyo, mapafu nipo vema na ninaamini kwamba nitaendelea kuwepo ndani ya Klabu ya Simba.

"Bado nipo ndani ya Simba kwa sasa, ninaomba taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa awali kuwa nitaondoka ndani ya Simba zipuuzwe," amesema.

8 COMMENTS:

  1. Nilijua kabisa unazuga tuu, Sijui wafuasi wako watakuelewaje?

    ReplyDelete
  2. Tulikuwa tukikuombea duwa na Mungu katusikia kinyume. na huyov hapo juu asiyetambuwa kudra za Mungu

    ReplyDelete
  3. Hana pa kwenda huyo nje ya simba hana cha maana cha kufanya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba ndo Chama kubwa, unataka awe utopolo? Manara kaza but I wanasimba tupo nawe siku zote

      Delete
  4. Bora ajastaafu, itapendenza akistaaafu kwa kufungwa either na Yanga au kutolewa Kwenye mashindano ya kimataifa ndio itanifaa.
    Muda huo ndio akapime kwa doctor Sasaiv hakuna pressure kwenda kupima ni kujipa moyo

    ReplyDelete
  5. Ukweli baada ya kumsikiliza Mo kwenye kipindi Cha mshike mshike Azam TV Jana,as from today sita comment issue za Haji sijui nani,nimegundua jamaa pamoja na kuipenda Simba anafanya biashara lkn anatambua kuwa mpira ni fairplay ,kumbe hata sajili nyingine wkt mwingine hajui ila anaheshimu watu walo mzunguka na hata Yanga ameiongelea kwa heshima tena kubwa, tatiZo ni Waganga njaa sijui ,Manara,pope na hizi media zilizojaa Usimba na TFF ,mwenzenu anasema mpira siyo uhasama wala ugomnvi lkn wengine mnaleta magubu ya home kwenu kwenye game so please tuheshimiane , appreciate analofanya mwenzako siyo kubweta kila siku

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic