August 19, 2020

 


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Farid Mussa, leo Agosti 19 ameanza mazoezi na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi nyingine za ushindani.


Farid ni ingizo jipya kwa msimu wa 2020/21 amesaini kandarasi ya miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake kwenye Klabu ya CD Tennerife ya Hispania alikokuwa akikipiga awali.

Yanga ilianza mazoezi Agosti 10 mapema kabisa kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria. Farid amesema:"Bado kuna nafasi ya timu kufanya vizuri, ahadi yangu kwa wananchi ni kupambana na kufanya vizuri zaidi."

Mchezo wa kwanza wa Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara utakuwa dhidi ya Tanzania Prisons, utachezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic