August 21, 2020

 


RASMI, kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Mghana, Bernard Morison, amekabidhiwa jezi namba tatu aliyokuwa anaivaa beki wa kati wa timu hiyo, Mbrazili, Tairone do Santos Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Mghana huyo ajiunge na Simba katika kuelekea msimu ujao akitokea Yanga akisaini mkataba wa miaka miwili.

 

Jumatatu ya wiki hii, Simba ilianza mazoezi kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena uliopo Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, huku mastaa wapya wa kimataifa walioanza mazoezi ni Chriss Mugalu, Larry Bwalya, Joash Onyango na Morrison.


Mghana huyo amekabidhiwa jezi hiyo baada ya Tairone kusitishiwa mkataba wake kutokana na kushindwa kumshawishi kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic