Nyota huyo amekuwa akihusishwa kuibukia ndani ya Klabu ya
Liverpool na Manchester United ambazo zimeonyesha kuwa zinahitaji saini yake jambo lililomfanya mchambuzi wa masuala ya michezo kituo cha ESPN raia wa Mexico, Sergio
Dipp kumwambia kwamba ni muda wake wa kupata changamoto mpya.
Jimenez amekuwa bora ndani ya Wolves akitupia jumla ya mabao 17
ndani ya Ligi Kuu England na mabao 10 ndani ya Europa League huku akitoa jumla ya pasi 10 za
mabao kwenye mashindano yote.
Raia huyo wa Mexico mwenye
miaka 29 ana nafasi ya kufanya makubwa msimu ujao kutokana na uwezo wake licha
ya timu yake kutolewa na Sevilla baada ya kufungwa bao 1-0 kwenye michuano ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Ni muda wake sasa kuondoka ndani ya Wolves na kwenda kupata
changamoto mpya kwenye timu kubwa, uwezo anao ikiwa ataondoka kwa sasa itampa
mabadiliko makubwa yeye mwenyewe mbeleni,”
0 COMMENTS:
Post a Comment