MENEJA wa Simba, Patrick Rweyemamu leo Agosti 7 amepokea Tuzo ya Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa niaba ya Meddie Kagere raia wa Rwanda ambaye amefunga mabao 22 ndani ya ligi.
Kagere kwa sasa yupo nchini Rwanda alikokwenda kwa ajili ya mapumziko mara baada ya ligi kukamilika.
Amekuwa ni mfungaji bora kwa misimu miwili mfululizo ambapo msimu wa 2018/19 alifunga jumla ya mabao 23 ndani ya ligi. Sherehe hizo zinafanyika leo ukumbi wa Mlimani City.
0 COMMENTS:
Post a Comment