August 27, 2020


KIUNGO mshambuliaji wa Namungo FC, Shiza Kichuya anasema bado ana matumaini ya kurejea kwenye kiwango cha juu kama ilivyokuwa zamani huku akisema kuwa ukosefu wa namba ndani ya Simba ni miongoni mwa sababu zilizomfanya akasepa.

 

Kichuya amejiunga kwa mkataba wa miaka miwili kwenye kikosi hicho chenye maskani yake Ruangwa mkoani Lindi akitokea Simba, anasema kikubwa ni kujituma na kufanya mazoezi kwa bidii.

 

“Naamini kuna wachezaji wazuri zaidi ndani ya Namungo, hivyo natakiwa kupambana ili kumwaminisha kocha na kunipatia nafasi ya kila mara kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

 

“Namungo ni timu kubwa ndio maana nimekuja huku, nikifanikiwa kupata namba kila wakati naamini kila mmoja atafurahi kwa kile nitakachokifanya uwanjani,” anasema Kichuya.

 

Mshambuliaji huyo ameongoza kusema licha ya mkataba wake kumalizika ndani ya Simba lakini ukosefu wa namba umechangia kuondoka kwake.


Akiwa Simba msimu wa 2019/20 alifunga bao moja kati ya mabao78 yaliyofungwa na timu hiyo ilikuwa Uwanja wa Mkapa wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting.

3 COMMENTS:

  1. Bora umeondoka,hapo ungeozea benchi. Tafuta namba ya kudumu uipiganie.........

    ReplyDelete
  2. Dah yote maisha maana kuna leo na kesho.Tatizo la wachezaji wetu watanzania wanapokuwa ktk hizi timu za kariakoo na Jangwani wanajisahau sana kufuata soka ethics na wanapoenda kucheza nje ya nchi wanajikuta wako nje na soka ethics zinavyotakiwa especially for proffesional player.Nakumbuka kuna kipindi cha kocha Omog amanusura Mkude apotee sababu ya hizi soka ethics.Alienda South Africa kwa majaribio ya kucheza soka lkn hatujui kilichofanya arejee nchini lkn nafikiri alijifunza kitu kuhusu proffesinal football player ethics ambazo zinatakiwa kuwa ndani na nje ya kiwanja.Tunamwona sasa Mkude anavyopambana na maisha yake ya soka na inabidi afanye hivyo kwani umri haudanganyi.Wako wachezaji wengi tena under 25 yrs lkn hatujui wameishia wapi zaidi ya kucheza Ndondo.Inasikitisha.Nimwambie Kichuya kujikwaa sio kuanguka na hivyo apambane asiangalie nyuma.Kila la kheri maestro Kichuya.

    ReplyDelete
  3. Kichuya kaza buti bado unaweza kufika mbali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic